‘Habari Njema kutoka kwa Mwenyezi

maana sana, atokaye katika kifua cha Mwenyezi Mungu,
hatuna budi kumjali kwa njia ya pekee, vinginevyo, sisi
nasi tutaonekana kuwa tunamtolea matusi makubwa sana
Mwenyezi Mungu.
Isa al-Masih alipokuwa kando ya mto Yordani ili
kubatizwa na kuwa kielelezo kwetu, Maandiko
yanatuambia sisi kwamba mbingu zikamfunukia na sauti
yake Mungu ikasikika … (Injili) Mathayo 17:5 ‘Alipokuwa
katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na
tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni
Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye;
msikieni yeye.’ Maneno hayo mawili ya mwisho,
‘msikieni yeye’ ni ya muhimu kwetu kwamba tusikilize
yale ambayo Mwenyezi Mungu ametuteremshia ndani ya
Isa al-Masih!
Injili, ambayo Muhammad alituambia kwamba
iliteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Sura 3:3, ina
mafungu ya maneno ya Maandiko ambayo yanarudia
kusema baadhi ya mawazo yale yale yapatikanayo katika
Sura 3:45 ambayo hunena juu ya Isa al-Masih kuwa ndiye
‘Neno aliyeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu’.
Angalia kile isemacho katika Yohana 1:1 ‘Hapo mwanzo
kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu
[Allah], naye Neno alikuwa Mungu [Allah].’ Kisha
inaendelea kutuambia sisi kwamba “Naye Neno alifanyika
mwili, akakaa [akateremshwa] kwetu” fungu la 14. Ni
huyu Neno aliyetuonesha sisi jinsi Mwenyezi Mungu
alivyo hasa.
Huyu si mwana aliyezaliwa kimwili kama watu leo
walivyo na watoto. Lakini huyu ni yule Mmoja aliyezaliwa
na bikira, ambaye alikuwa bado hajamjua mume.
Kumbuka kwamba hakuna neno lo lote lililo gumu kwa
Mwenyezi Mungu! Yeye aweza kusema tu na mambo
yakawa vile. Soma tena Sura 3:46
Je! huyo ni Mwanawe Mungu (Allah)?
Huenda umewahi kusikia usemi huu “mwana wa njia”, je,
njia ina mwana? La, hasha, lakini maana yake hapa ni
kwamba mtu yule anayekidhi maelezo hayo ni msafiri.
Usikate tamaa unaposikia kifungu hiki cha maneno “Kristo,
Mwana wa Mungu” hii haimanishi kwamba Mungu [Allah]
anaye mwana aliyemzaa kwa njia ile ile wanadamu
wanavyozaa watoto, kwa maana hilo kamwe haliwezi kuwa
hivyo. Lakini kinamtaja Kristo kuwa ni Mwana kwa
maana ile ambayo Isa yuko karibu sana na Mwenyezi
Mungu na ni kwa njia ya Isa (Kristo) tabia ya Mwenyezi
Mungu inadhihirishwa kwetu vizuri sana. Njia iliyo wazi
kabisa na bora kabisa kwa Mwenyezi Mungu kuwasiliana
na wanadamu ni kumtumia mmoja anayefanana na sisi!
Hivyo Yeye ndiye Neno kutoka kwa Mwenyezi Mungu
…”msikieni yeye”.
Kichaka Kilichowaka Moto
Mpendwa rafiki usifikiri hata kwa dakika moja kwamba
Mwenyezi Mungu amewekewa mipaka na hawezi kufanya
hili. Kumbuka kisa cha Musa na kichaka kilichowaka
moto. Kinatuambia kwamba Mwenyezi Mungu alinena na
Musa kutoka katika ule moto. Kama Mwenyezi Mungu
anaweza kuja kwa mfano wa kichaka kinachowaka moto,
je! hawezi pia kuja katika umbile la Mwanadamu na
kujidhihirisha Mwenyewe kwetu na kunena nasi? Ni
hakika kabisa hakuna kitu cho chote kilicho kigumu kwa
Mwenyezi Mungu!
Mwenyezi Mungu na akubariki sana unapotafuta kufanya
mapenzi yake na kuchagua kutii kile alichokudhihirishia
wewe. Ni kweli Neno kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndani
ya Kristo Masihi hizo kwetu ni “Habari Njema” ‘msikieni
yeye’! Bismillahir rahmanir rahim”.
Kabla hujafungua kurasa za Vitabu Vitakatifu, daima omba
Mwenyezi Mungu akufundishe kuwa na ufahamu sahihi
usomapo. Mwenyezi Mungu anawabariki wale
wanaojifunza kwa unyofu wa moyo na wanaoitafuta haki.
Yeremia 29:13 ‘Nanyi mtanitafuta, na kuniona,
mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.’ Wale wamtafutao
Mwenyezi Mungu, hawana budi kumtafuta kwa moyo wao
wote.
Al-Baqara 002.153
‘Enyi mlioamini! Jisaidieni (katika mambo yenu) kwa
subira na Sala; bila ya shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja
na wanaosubiri.’
Aya zimenukuliwa kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer
software v2.913
Mafungu ya Biblia kutoka Toleo la King James (KJV)
Kwa maelezo zaidi au mauidha tafadhali wasiliana
na:
www.salahallah.com